MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA ASA NANENANE - DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametembelea banda la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John S. Malecela, Nzuguni mkoani Dodoma.
Katika ziara hiyo, Mhe. Makamu wa Rais alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na ASA, ikiwemo uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za mazao ya kilimo, pamoja na jitihada za Serikali za kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora kwa wakati ili kuongeza tija na usalama wa chakula nchini.
Mtendaji Mkuu wa ASA alimueleza Makamu wa Rais kuhusu aina mbalimbali za mbegu zinazozalishwa na Wakala, maeneo ya uzalishaji, pamoja na mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima katika mikoa yote ya Tanzania.
Maonesho ya Nane Nane 2026 yanafanyika kitaifa Dodoma na kanda zote nchini kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2026 na yanawakutanisha wadau wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kutoka ndani na nje ya nchi.
#MbeguBora #KilimoKwanza
PICHA YA PAMOJA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO (ASA).
UZINDUZI WA KAMATI YA UKAGUZI YA WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO (ASA) MAKAO MAKUU MJINI MOROGORO
ASA YASHIRIKI WIKI YA MAADHIMISHO YA CHAKULA MKOANI TANGA.
PICHA YA PAMOJA YA KAIMU MTENDAJI MKUU WA ASA (WATATU KUTOKA KULIA) , WAKUFUNZI NA WAFANYAKAZI MBALIMBALI WA ASA WAKIWA KATIKA MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI YA VIUWATILIFU NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KUPITIA MPANGO WA KUSTAHIMILI MFUMO WA CHAKULA TANZANIA (TFSRP).
ASA YAENDELEA KUNUFAIKA NA MRADI WA AFDP KUPITIA PROGRAM YA IFAD
ASA YAKABIDIWA ENEO LA HEKTA 240 (SAWA NA EKA 601) IKIWA SHAMBA LA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KILIMO
MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI (BWAWA) SHAMBA LA MBEGU ZA KILIMO LA ASA, ARUSHA- NGARAMTONI
ASA KUSHIRIKIANA NA TFC KUONGEZA UZALISHAJI NA USAMBAZAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO NCHINI
PICHA YA PAMOJA BODI YA USHAURI ASA NA MENEJIMENTI YA ASA
ASA was established under the Executive Agencies Act [Cap.245 R.E. 2002]. The Agency was launched in June 2006 as a semi-autonomous body under the Ministry of Agriculture...