ASA YAZINDUA RASMI KAMATI YA UKAGUZI WA NDANI
24 Oct, 2025
ASA YAZINDUA RASMI KAMATI YA UKAGUZI WA NDANI

Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA), leo tarehe 24 Oktoba 2025 yazindua kamati ya ukaguzi wa ndani makao makuu  mjini Morogoro.

Kamati hiyo imezinduliwa na  Mtendaji Mkuu wa ASA Bw. Leo Martin Mavika sambamba na Mwenyekiti wa kamati hiyo  CPA Daniel John Mark pamoja na wajumbe mbalimbali na timu ya menejimenti ya ASA. 

Katika uzinduzi huo kamati ilipitia na kujadili taarifa mbalimbali ikiwemo nyaraka za Kamati ya Ukaguzi ambazo ni audit committee charter na mpango kazi wake, nyaraka za kitengo cha ukaguzi wa ndani ambazo ni internal audit charter, mpango mkakati wa miaka mitatu (strategic internal audit plan) ya miaka 2025/26 mpaka 2027/28, mpango kazi wa mwaka (risk based internal audit plan) wa mwaka 2025/26, pamoja na taarifa ya ukaguzi wa ndani wa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/26