
Dr. Sophia Kashenge-Killenga
NENO LA MTENDAJI MKUU!
Usalama wa nchi yeyote ni usalama wa chakula. Wakati huohuo usalama wa chakula hujengwa na uwepo wa usalama na matumizi sahihi ya mbegu bora. Ukuaji wa sekta ya kilimo huenda sambamba na matumizi ya technolojia bora ikiwemo mbegu bora za Kilimo.
Serikali pia ilianzisha kwa makusudi kabisa wakala wa Taifa wa uzalishaji na uendelezaji wa mbegu za kilimo (ASA) ili kuhakikisha usalama wa chakula nchini unabaki mikononi mwa serikali kwa maana ya usalama wa mbegu. Kimsingi katika jukumu hili la uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za kilimo ASA kama taasisi ya serikali ni imeazimia kuhakikisha azma ya serikali kufuka kwenye uchumi wa viwanda kupitia kilimo inatimia.
Majukumu ya ASA mbali na kuhakikisha mbegu bora zinapatikana na kuwafikia wakulima kwa wakati na kwa bei iliyo nafuu, inajukumu pia la kuzinadi kwa nguvu mbegu zinazozalishwa na zinazotengenezwa na vituo vya utafiti. ASA ina mikakati mingi katika kujikwamua kwenye changamoto mbalimbali zinazopunguza kasi ya maendeleo ya tasnia ya mbegu nchini, ikiwemo kutumia fursa mbalimbali Aidha pia wakala unajukumu kubwa la kufanya kazi na sekta binafsi hasa makampuni binafsi ya mbegu ili kuhakikisha uwepo wa ongezeko la upatikanaji wa mbegu bora kwa mkulima wa nchi hii na kupunguza changamoto ya ukosefu wa mbegu bora nchini.
Mashamba yake 9 ya mbegu yaliyotawanyika katika kanda zote za kilimo nchini. Moja ya jukumu la ASA ni kushirikiana na makampuni binafsi (Public-Private partinership) katika kuongeza kazi ya uzalishajiwa mbegu nchini. Ili kukamilisha jukumu hili la kushirikiana na makampuni binafsi, baadhi ya makampuni hutumia rasilimali za ASA iliwemo ardhi, mashine za uchakataji wa mbegu na mitambo ili kuzalisha mbegu zao na kuziuza kwa wakulima, baadhi ya makampuni pamoja na wakulima wa mkataba huzalisha mbegu na kuiuzia ASA. Baadhi ya makampuni hayo pia hununua mbegu za msingi kutoka ASA na kuzizalisha na baadaye kuziuza kwa wakulima, katika ubia huu na makampuni binafsi ASA pia inashirikiana katika kubadilishana uzoefu na kupeana elimu katika nyanja za uzalishaji, uchakataji na uhifadhi wa mbegu bora. Aina hii ya ubia ni muhimu sana kwa maendeleo ya Tasniaya mbegu na Kilimo kwa ujumla. Hivyo, ASA ina fursa mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa na wadau mbalimbali katika Tasnia ya mbegu lengo likiwa ni kuongeza kasi ya uzalishaji wa mbegu bora nchini.
OUR PRODUCTS
ALIZETI
SESAME
LOSHUU
Situka-M1
Onion-Mangola-Red
Tomato-Tanya
Saro-5-TXD-306
Tomato-Tengeru
LATEST NEWS
ASA WATOA MBEGU ZA NGANO MAKETE
Njombe.
Serikali ya Tanzania imeanza jitihada za kukabiliana na upatikanaji wa zao la Ngano kwa kuanza rasmi uzalishaji wa zao
Dkt,SOPHIA AWAASA VIJANA WA VYUO VIKUU NA VYAKATI
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt, Sophia Kashenge amewataka Vijana kuingia katika sekta ya kilimo huku
WAZIRI BASHE ATOA MAELEKEZO KWA ASA
Waziri wa Kilimo Mhe,Hussein Bashe akitoa Maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu Dr,Sophia Kashenge katika Shamba
ASA YA POKEA MTAMBO WA KUCHAKATA MBEGU
Baadhi ya watumishi wa wakala wa Mbegu za Kilimo ASA katika Shamba la Mbegu Msimba wakishusha Mtambo wa kuchakata Mbegu
ASA KUTOA MICHE 20,000 YA PARACHICHI AINA YA HASS
Waziri wa Kilimo Mhe,Hussein Bashe akizungumza na wadau wa zao la chai Mkoani Iringa katika ziara yake ya kikazi