ASA YATOA HUDUMA YA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO KWA WAKULIMA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA CHAKULA MKOANI TANGA.
Wakala wa mbegu bora za kilimo (ASA), yashiriki katika maadhimisho ya wiki ya chakula Duniani yanayoendelea mkoani Tanga yaliyoanza tarehe 10 hadi kilele 16 oktoba 2025,
ASA inaendelea kuhakikisha upatikanaji na utoaji wa elimu ya matumizi sahii ya mbegu bora za kilimo kwa wananchi ili kuongeza uzalishaji wenye tija na usalama wa chakula nchini kwa wakazi wa Tanga na vitongoji vyake.
Maadhimisho haya yaliyofunguliwa leo tarehe 11 oktoba 2025 na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Mhe. Batlida Salha Burian na kuambatana na Dkt. Stephen J. Nindi Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula) na viongozi mbalimbali wa mkoa.
Maadhimisho yenye kauli mbiu “Tuungane pamoja kupata Chakula Bora kwa Maisha Bora ya baadae”, yanayotarajiwa kufika tamati tarehe 16 oktoba 2025 na mgeni ramsi ni Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jahmhuri ya Muungano wa Tanzania.
