Mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu na utunzaji wa mazingira kupitia mpango wa kuhimili Mifumo ya Chakula Tanzania (TFSRP).

BW. MAVIKA AISHUKURU WIZARA YA KILIMO KWA KUPENDEKEZA ASA KATIKA UTEKELEZA WA PROGRAMU YA TFSRP
Na Mwandishi wetu- Morogoro
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Bw. Leo Mavika ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa kupendekeza ASA katika utekelezaji wa Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula Tanzania (TFSRP)
Shukrani hizo zimetolewa leo Septemba 13, 2025 na Bw. Mavika wakati akifunga mafunzo ya Matumizi sahihi ya Viuwatilifu na utunzaji wa Mazingira kupitia Program ya Mifumo himilivu ya Chakula Tanzania (TFSRP).
Bw. Mavika amesema, mafunzo haya ni muhimu kwetu ili kuongeza uzalishaji wenye tija na kutunza mazingira.
"Mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kufanya Matumizi sahihi ya Viuwatilifu na utunzaji wa Mazingira mashambani, hii itachochea mazingira rafiki ya uzalishaji wa mbegu bora za kilimo na tija" amesema Bw. Mavika na kuongeza kuwa
“Naishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya Sekta ya Kilimo” amesema Bw. Mavika
Pia amemshukuru Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) na menejimenti ya wizara ya kilimo kwa kuipambania Sekta ya kilimo na kuleta mageuzi makubwa ya kilimo hapa nchini kwa kusimamia vema upatikanaji wa fedha kwaajili ya programu hii na shughuli mbalimbali za kilimo ikimo kuipendekeza ASA katika utekelezaji wa mradi huu wa TFSRP”