ASA YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA YA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO KWA WAKULIMA KATIKA MAONESHO YA KILIMO YA SAMIA KILIMO BIASHARA EXPRO 2025, GAIRO.
Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA), imesogeza huduma yake ya upatikanaji wa mbegu bora za kilimo katika maonesho ya Nne ya SAMIA KILIMO BIASHARA yanayofanyika Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wakulima katika wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro wamefurahishwa na huduma hiyo ya upatikanaji wa Mbegu bora za kilimo karibu kutoka (ASA), baada ya kupatiwa elimu ya namna bora ya matumizi ya Mbegu zilizothibitishwa ili kuongeza uzalisha wenye tija kwa wakulima nchini.
Mbegu hizo ambazo ni Mahindi aina ya T 105 inayovumilia ukame,Magonjwa na wadudu hali iliyowafanya Wakulima hao kuchangamkia fursa ya kununua Mbegu hizo iliwaweze kupata Mazao mengi na yenye tija.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Kissa Kasongwa, ameipongeza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa kusogeza huduma ya upatikanaji wa Mbegu bora za kilimo kwa wakulima na kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya Mbegu kwani elimu hiyo itaongeza kipato kwa mkulima na kumwinua kiuchumi.
Wakala wa mbegu za kilimo (ASA), wanashiriki katika maonesho ya Samia Kilimo Expo katika wilaya ya Gairo ikiwa ni msimu wa nne.
