DC NYANGASA ATEMBELEA BANDA LA ASA NANENANE, ATOA WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU BORA ZA ASA
DC NYANGASA ATEMBELEA BANDA LA ASA NANENANE, ATOA WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU BORA ZA ASA
01 Aug, 2025
4:00 - 12:00
NZUNGUNI, DODOMA
info@asa.go.tz
DC NYANGASA ATEMBELEA BANDA LA ASA NANENANE, ATOA WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU BORA ZA ASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Mhe. Fatma Almas Nyangasa ametembelea banda la Wakala wa Mbegu za Kilimo katika Maonesho ya wakulima ‘Nanenane’ yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma, ambapo ametoa wito kwa wakulima katika matumizi ya mbegu za kilimo ili kupata mazao yenye tija.
Akizungumza katika banda hilo, leo Jumatano Agosti 06, 2025 Mhe. Fatma Almas Nyangasa ameipongeza ASA kwa kazi kubwa ya kutoa huduma ya kupata na elimu ya mbegu bora kwa wakulima nchini, na kutoa wito Kwa wakulima kutumia mbegu bora za ASA.
