MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA ASA NANENANE - DODOMA
26 Aug, 2026
MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA ASA NANENANE - DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametembelea banda la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John S. Malecela, Nzuguni mkoani Dodoma.

Katika ziara hiyo, Mhe. Makamu wa Rais alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na ASA, ikiwemo uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za mazao ya kilimo, pamoja na jitihada za Serikali za kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora kwa wakati ili kuongeza tija na usalama wa chakula nchini.

Mtendaji Mkuu wa ASA alimueleza Makamu wa Rais kuhusu aina mbalimbali za mbegu zinazozalishwa na Wakala, maeneo ya uzalishaji, pamoja na mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima katika mikoa yote ya Tanzania.

Maonesho ya Nane Nane 2026 yanafanyika kitaifa Dodoma na kanda zote nchini kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2026 na yanawakutanisha wadau wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kutoka ndani na nje ya nchi.

#MbeguBora #KilimoKwanza